Uwanja wa Benjamin Mkapa ni miongoni mwa viwanja vitatu vya Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) vilivyopitishwa kutumika kwenye raundi ya kwanza na raundi ya pili ya michezo ya kufuzu fainali za Mataifa bingwa Afrika CHAN.
–
Viwanja vingine vya Kanda ya CECAFA ambavyo navyo vimethibitishwa ni St Mary’s, Uganda na Al Hilal, Sudan.
–
Michezo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa kati ya Julai 22-24, 2022 na michezo ya marudiano itachezwa kati ya Julai 29-31, 2022.
–
Tanzania imepangwa kuanza na Somalia kwenye raundi hiyo ya kwanza ya mashindano hayo ambayo yanahusisha wachezaji wa ndani.