Mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole, amefanikiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ kwa idadi ya mabao 17.
–
Hii ni baada ya kufunga bao lake la 17 katika sare 1-1 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Mkwakwani.
–
Nafasi ya pili imechukuliwa na Fiston Mayele akiwa na mabao 16 ambapo amekosa kiatu hicho baada kushindwa kufunga bao wakati Yanga ikiifunga Mtibwa Sugar 1-0.
–
Katika dakika zake 2,427 alizotumika dimbani msimu huu, straika wa Geita Gold, George Mpole amehusika katika magoli magoli 21 kati ya magoli 32 yaliyofungwa na timu yake. Huyu ndiye mfungaji bora wa msimu huu akiwa amefunga magoli 17, assist 4