Mtoto wa miaka miwili(2) Nkiya Thomas, Mkazi wa Kijiji cha Nyamigogwa Kata ya Shabaka Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita, amekutwa ameuawa kwa kuchinjwa na Watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye shamba ambalo lipo mkabala na nyumba yao.
–
Jamhuri David ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuagiza uchunguzi wa tukio hili ufanyike haraka “Hatuwezi kukubali Wilaya yetu kuwa na matukio ya namna hii , kwa upande wangu nimesikitishwa sana na tukio hili niombe tushirikiane kutokomeza haya matukio”
–
Kwa upande wake Mama Mzazi wa Mtoto aitwaye Mperwa Sahani amesema “Taarifa ya kifo cha Mtoto wangu nilipewa na Mtoto wa Shemeji yangu kuwa Nkiya amefariki wamemuona shambani amechinjwa nilipofika kweli nilikuta Mtoto wangu amechinjwa”
Credit – Millard Ayo