ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, June 29, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

MZEE MAARUFU ‘MARIA NTOWE’ , MCHIMBAJI MADINI ANAYEHAMASISHA WANAWAKE KUKAMATA FURSA ZA KIUCHUMI

I am Krantz by I am Krantz
Jun 6, 2022
in HABARI
0
MZEE MAARUFU ‘MARIA NTOWE’ , MCHIMBAJI MADINI ANAYEHAMASISHA WANAWAKE KUKAMATA FURSA ZA KIUCHUMI
0
SHARES
27
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

Jun 29, 2022

POLISI 156 WAFUKUZWA MAFUNZONI

Jun 29, 2022

VIGOGO WA CHAMA CHA WALIMU WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA

Jun 29, 2022
Load More
Mzee Maarufu Bi. Maria Stephen Ntowe (70) akielezea namna alivyotumia fursa ya uchimbaji madini kujipatia kipato na kujiinua kiuchumi baada ya kupewa mafunzo ya kujiamini na kuchukua fursa za kazi zinazofanywa na wanaume kwani na wanawake wanaweza kuzifanya kwenye kikao cha mrejesho wa Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya Msalala mkoani Shinyangakwa kuhusu masuala ya Kisheria na kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao kilichoandaliwa na TGNP kupitia UNFPA kwa ufadhili wa KOICA. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mzee Maarufu Bi. Maria Stephen Ntowe (70) akielezea namna alivyotumia fursa ya uchimbaji madini kujipatia kipato na kujiinua kiuchumi.
Mzee Maarufu Bi. Maria Stephen Ntowe (70) akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika jamii ambapo sasa wanawake wanashiriki shughuli za uchimbaji madini kwenye kikao cha mrejesho wa Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya Kisheria na kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao kilichoandaliwa na TGNP kupitia UNFPA kwa ufadhili wa KOICA.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao cha mrejesho wa Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya Kisheria na kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Shinyanga, John Shija ambaye ni Mratibu wa shughuli zinazofanywa na TGNP Mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao cha mrejesho wa Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuhusu masuala ya Kisheria na kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao.


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mzee Maarufu Bi. Maria Stephen Ntowe (70) mkazi wa kijiji cha Lunguya kata ya Lunguya Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga amewataka wanawake kuchangamkia fursa ya uchimbaji madini ili waweze kujipatia kipato na kujiinua kiuchumi kwani sasa ile ya mila potofu kuwa Wanawake wakiingia katika migodi wanaleta mikosi imepotea hivyo shughuli za uchimbaji madini zinafanywa na wanaume na wanawake.

Bi. Maria ametoa rai hiyo Jumamosi Juni 4,2022 kwenye kikao cha mrejesho wa Wasaidizi wa Kisheria na Vituo vya Taarifa na Maarifa kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya Msalala mkoani Shinyangakwa kuhusu masuala ya Kisheria na kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwa ni mwendelezo wa kazi ya Mradi wa Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wananchi kiuchumi Mkoa wa Shinyanga katika halmashauri ya Msalala unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kupitia Shirika la Kimataifa la UNFPA kwa ufadhili wa KOICA.

Bi. Maria ambaye pia ni Mhasibu wa Wazee Halmashauri ya Msalala amesema kazi ya kuchimba madini ni kazi ya jinsi zote hivyo wanawake na wanawake wanayo nafasi ya kushirikiana na wanaume kuchimba madini.


“Zamani tulikuwa tunaambiwa kuwa wanawake tuna mikosi kama mti uitwao ‘Mzima’ kwamba tukiingia mgodini dhahabu inakimbia .Mti wa Mzima hauruhusiwi kuonekana mgodini kwa sabab unaaminika kuzima bahati hivyo wanawake tulifananishwa na mti huo kwamba ni mkosi kuonekana mgodini lakini sasa mambo yamebadilika hizo mila na imani potofu zimepungua wanawake wengi sasa wanashiriki shughuli za uchimbaji madini“,ameeleza Bi. Maria.


ALIANZAJE SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MADINI


Bi. Maria anasema alipata hamasa ya kuanza shughuli za uchimbaji madini baada ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kuanza kutekeleza shughuli zake katika kata ya Lunguya na Shilela halmashauri ya Msalala Oktoba 2020 ambapo TGNP ilikutana na wanawake na kuwapa mafunzo jinsi ya kujiamini na kuchukua fursa za kazi zinazofanywa na wanaume kwamba hata wanawake wanaweza kuzifanya.


“Mwanzo niliona ni kama ndoto wanawake kuwa wachimbaji baada ya kupata mafunzo ya TGNP nilipata ujasiri na kujiamini kuwa naweza kufanya kazi zinazofanywa na wanaume, nikaona fursa ya kiuchumi na nilivutiwa na wanawake ambao tayari walikuwa wameanza shughuli za uchimbaji na sasa naendelea kunufaika na kazi hii. Na sasa naamini kuwa wanawake tunaweza kumiliki rasilimali zetu na zikatusaidia kujiinua kiuchumi”, amesema Bi. Maria.

Bi. Maria ambaye ni mkazi wa Lunguya anayemiliki duara tatu katika mgodi wa dhahabu wa Nyamishiga kata ya Lunguya anasema alianza shughuli za uchimbaji madini mwaka 2020 kwenye shamba lake na kuanza kumiliki duara katika mgodi huo mwezi Januari 2022 alipojiunga na kikundi cha wachimbaji.


“Kuwa mchimbaji wa madini siyo lazima uwe unachimba mwenyewe bali unaweza kujiunga katika kikundi na badala ya kuchimba unatoa pesa kama mimi ninavyofanya, ukitoa fedha unakuwa mwanachama wa kikundi, nina maduara yangu matatu wanachimba wengine lakini mali inayopatikana nanufaika nayo”, amesema Bi. Maria.


Mzee huyo maarufu amesema pia anatumikia Idara ya Felo (mawe ya dhahabu yenye hali ya chini) ambapo majukumu yake ni kuweka nembo kwenye mifuko inayobeba mawe hayo.


Amewahamasisha wanawake kujiamini na kuchangamkia fursa za uchumi zilizopo kwenye maeneo yao ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia unaosababishwa na hali duni ya kiuchumi katika kaya.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA
HABARI

R KELLY AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
POLISI 156 WAFUKUZWA MAFUNZONI
HABARI

POLISI 156 WAFUKUZWA MAFUNZONI

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
VIGOGO WA CHAMA CHA WALIMU WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA
HABARI

VIGOGO WA CHAMA CHA WALIMU WAHUKUMIWA MIEZI 6 JELA

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
MAHAKAMA YATOA AMRI KESI HALIMA MDEE NA WENZAKE
HABARI

MAHAKAMA YATOA AMRI KESI HALIMA MDEE NA WENZAKE

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI HUU
HABARI

RAIS SAMIA ATEUA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022
MPOLE AMFUNIKA MAYELE LIGI KUU YA NBC 2021/22
HABARI

MPOLE AMFUNIKA MAYELE LIGI KUU YA NBC 2021/22

by Shabani Rapwi
Jun 29, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In