
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
NCHI ya Uturuki imefikia uamuzi wa kubadili jina lake linalotambulika siku zote la Turkey na sasa itafahamika kama Turkiye.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mwaka jana mwezi desemba alisema:
“Turkiye ni kielelezo na kiwakilishi kizuri cha utamaduni, ustaarabu na thamani ya raia wa Uturuki.”
Umoja wa Mataifa umebainisha kuwa tayari umeshafanya mabadiliko mara tu baada ya kupokea taarifa hiyo mapema wiki hii.
Raia wengi wa Uturuki tayari wanaitambua nchi yao kwa jina la Turkiye ingawa changamoto iliyopo ni kwamba jina la mwanzo bado ni maarufu sana midomoni mwa watu.

Rais Erdogan amesema jina la Turkiye ni kielelezo halisi cha raia wa Uturuki
Kituo cha Utangazaji cha Taifa TRT kilifanya mabadiliko ya haraka mara tu baada ya mchakato kutangazwa mwezi desemba mwaka jana.
Siyo jambo la ajabu au la kushangaza kwa nchi kubadili jina kwani tayari kuna mifano kadhaa ya nchi ambazo tayari zimeshabadili majina yao kwa sababu mbalimbali.
Nchi ya Uholanzi ilibadili jina lake kutoka Holland na kuwa Netherlands, Marcedonia ilibadili jina na kuwa North Macedonia, Iran ya sasa ilikuwa ikiitwa Persia huku Zimbabwe ya sasa zamani ilikuwa ikifahamika kama Rhodesia.