KIUNGO wa Simba aliyepo kwa mkopo wa miezi sita Mtibwa Sugar, Said Ndemla muda wowote huenda akasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Singida Big Stars (zamani DTB).
–
Awali, Ndemla alikuwa akihusishwa na Azam, lakini imeelezwa amebadili gia angani na kuchomokea Singida iliyopanda Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao ikitoka Ligi ya Championship.
–
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Mtibwa ilimchukua Ndemla kwa mkopo kutoka Simba mwanzoni mwa msimu huu na mwishoni mwa ligi atamaliza mkataba huo na inaelezwa tayari ameshamalizana na Singida.