Msanii wa Bongofleva, Mimi Mars amefunguka sababu za kuimba nyimbo za mapenzi mara kwa mara kuwa ni kutokana na kuumizwa kimapenzi.
Alikiri amefanya kazi nyingi zinazohusu mapenzi tangu ameanza muziki kutokana anapenda mapenzi lakini yamekuwa yanamuumiza.
“Ni mwanamke, nimeshavuka miaka 18, nilishakuwa kwenye mahusiano na nimeumizwa sana kwenye sekta hiyo, naweza kusema ndio sababu ya kufanya kazi nyingi zinazohusu mapenzi” amesema.
Kwa sasa Mimi Mars anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la La La ambao amemshirikisha Marioo anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha hilo.
cc @mimi_mvrs11