Msaani wa Muzik kutoka lebo ya WCB Wasafi, Mbwana Yusuf Kilungi maarufu Mbosso akiwa kwenye Mahojiano na kituo cha radio, Wasafi FM amefunguka, kusumbuliwa na tatizo la Moyo ambalo limekuwa likimtesa siku nyingi japo ni wachache ambao wanafahamu hilo.
–
“Nina Matatizo makubwa sana ya Moyo yananitia unyonge sana naweza nikalala usiku nashtuka upande wa kushoto unauma sana, Ni maradhi ambayo yananisumbua muda mrefu sana”
–
“Mimi Mzito sana kuongea vitu vyangu, maradhi yangu yamesababishwa na kuziba mafuta kwenye Mishipa ya Moyo na Wataalam wamesema nisipotibiwa naweza nisizae” alisema Mbosso