Klabu ya Zulte Weregem ya Ubelgiji, imetangaza kumsajili kiungo Mtanzania, Novatus Dismas, kutokea Macabi Tel Aviv ya Israel.
–
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, ameingia mkataba wa miaka mitatu kuitumikia timu hiyo ambayo imewahi kushinda taji la Belgian Cup mara mbili.
–
ADVERTISEMENT
Novatus atakuwa ni mtanzania wa tatu kusajiliwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji “Belgian Jupiler Pro League” baada ya Mbwana Samatta aliyekuwa anakipiga Royal Antwerp kwa mkopo na Kelvin John ambaye anakipiga kwenye klabu ya KRC Genk.
ADVERTISEMENT