ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, October 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

NYANI WAPORA MTOTO MCHANGA

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Jun 20, 2022
in HABARI
0
NYANI WAPORA MTOTO MCHANGA
0
SHARES
316
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

 

RelatedPosts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

Sep 29, 2023

TSO WAZINDUA GALA DINNER

Sep 29, 2023

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

Sep 29, 2023
Load More

 

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema kuwa kundi la nyani wa hifadhi ya Gombe iliyopo kijiji cha Mwamgongo wilayani Kigoma, limevamia nyumba ya Shayima Faya (20) na kumpokonya mtoto mchanga wakati akimnyonyesha na kutokomea naye porini ambapo baadaye mtoto huyo alifariki dunia.

 

–

 

 

Akizungumza na waandishi wq habari leo Jumatatu Juni 20, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Juni 18, 2022 katika kijiji hicho.

 

–

 

 

Amesema baada ya tukio hilo mwanamke huyo alipiga kelele  kuomba msaada na majirani walijitokeza kumdhibiti mnyama pori huyo ambaye alimtupa mtoto huyo chini akiwa tayari amejeruhiwa kichwani, usoni na mguu wa kushoto.

 

–

 

 

“Wananchi walifanikiwa kulikimbiza kundi hilo la nyani lililomvamia mwanamke huyo wakati akimnyonyesha wanaye,  na kufanikiwa kumpata mtoto akiwa amejeruhiwa lakini baada ya kufikishwa kituo cha afya Mwamgongo alifariki dunia,”amesema Manyama.

 

–

 

 

Katika tukio jingine watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki na visu walivamia duka la mfanyabiasha Livingston Godluck (35) na kupora Sh5 milioni pamoja na simu za mkononi ambazo bado hadi sasa thamani yake hazijafahamika.

 

–

 

 

Kamanda Manyama amesema tukio hilo limetokea Juni 19, 2022 eneo la stendi ya zamani kata ya Kibondo  wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

 

–

 

 

Amesema katika tukio hilo wanamshikilia mtu mmoja mwenye miaka 25, walimkamata porini akiwa amejeruhiwa na risasi na baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na kuwataja wenzake ambao walifanikiwa kutoroka na kurudi nchini Burundi.

Related

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Related Posts

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO
HABARI

CHAGUZI KUFANYIKA MTANDAONI SIKU ZIJAZO

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TSO WAZINDUA GALA DINNER
HABARI

TSO WAZINDUA GALA DINNER

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
CHANJO YA MBWA NI MUHIMU
AFYA

CHANJO YA MBWA NI MUHIMU

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN
HABARI

52 WAFARIKI KWENYE MAADHIMISHO YA MAULID NCHINI PAKISTAN

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA
HABARI

SEKTA YA MADINI YAJA NA MBT KAMA FURSA KWA VIJANA

by SUZO SHUKRANI
Sep 29, 2023
TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 
HABARI

TUNZAA YATANGAZA USHIRIKIANO MKUBWA NA KAMPUNI YA VODACOM KUPITIA M-PESA 

by I am Krantz
Sep 29, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May   Jul »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In