Beki kisiki wa Simba, Joash Onyango amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2020 akitokea Gor Mahia ya Kenya.
–
Onyango ambaye pia ni beki wa timu ya Taifa Kenya ‘Harambee Stars’ akizungumza na gazeti la Nation nchini Kenya amesema ameongeza mkataba na uongozi utatoa maelezo zaidi.
–
Beki huyo mwenye miaka 29 kabla ya kusaini alitoa masharti mapya ya mkataba wake mpya ambao uongozi umesema hayajatimizwa yote ila umeboreshwa.