Kituo cha Habari cha EFM kimempa mkono wa kwaheri mchambuzi wake, Oscar Oscar baada ya kukitumikia kwa miaka saba.
–
Kupitia kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram, EFM imemshukru mchambuzi huyo na kumtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mpya.
–
“Oscar Oscar ni mmoja wa wachambuzi waandamizi ambao wamekuwa nasi kwenye Sports HQ kwa miaka 7 sasa. Sisi tunamshukuru kwa uchambuzi wa kina, vituko, maoni na yote aliyofanya kwenye kipindi hicho. Tunamtakia kila lenye kheri kwenye majukumu yake mapya”.