ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Kocha Pitso Mosimane ameondoka kwa wababe wa Misri, Al Ahly baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.
–
Al Ahly wamethibitisha kuondoka kwa kocha huyo kupitia kwenye tovuti yao rasmi.
–
“Mahmoud El Khatib, rais wa klabu, alifanya mkutano na Yassin Mainsour, mwenyekiti wa Kampuni ya Soka ya Al Ahly; Hossam Ghaly, mjumbe wa bodi ya klabu na wajumbe wa kamati ya mipango, kujadili mustakabali wa Mosimane na klabu hiyo.
–
“Waliamua aendelee na majukumu yake kutokana na mafanikio makubwa aliyeyapata” “Hata hivyo katika kikao kilichofanyika awali Mosimane aliomba kuondoka na [alisema] kwamba ameridhishwa na mafanikio aliyoyapata kwenye klabu”.