Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amesema askari polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa kwenye mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya polisi.
–
IGP Sirro amesema hayo alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilayani Siha, West Kilimanjaro katika shule ya polisi Tanzania.
–
Pia amewaelekeza wanafunzi wa kozi ya awali ya askari polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya jeshi la polisi.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT