Mbunge wa Jimbo la Ubungo mkoani Dar es Salaam (CCM) Profesa Kitila Mkumbo amekabidhi fedha za ada kwa wanafunzi 61 waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi hususan somo la hesabu, katika mitihani wa kidato cha nne ya mwaka 2021.
–
Profesa Kitila amekabidhi zawadi hizo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi yale kwa walimu na wanafunzi kupitia motisha aliyoitoa ndani ya jimbo hilo katika kusaidia ongezeko la ufaulu wa masomo ya sayansi pamoja na ubora wa ufundishaji.
–
Amesema katika utafiti uliohusisha hali ya elimu katika jimbo hilo umeonyesha kuwa katika wanafunzi 100, wanafunzi 11 pekee ndio waliokuwa wanafaulu hesabu hivyo hali hiyo ilimsukuma kuweka kipaumbele cha elimu huku akianzisha motisha kwa walimu na wanafunzi kwa kutoa zawadi ili kuchochea kiu ya kufundisha na ufaulu kwa wanafunzi.