Baada ya kutolewa kwa pendekezo kuwa R kelly anapaswa afungwe kifungo cha miaka 25 jela, mmoja wa waathirika wa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia anae fahamika kwa jina la Lizzete Martinez amesema, miaka hiyo ni michache mno ukilinganisha na makosa aliyoyafanya.
–
Lizzette anafikiri kwamba pendekezo la shirikisho la miaka 25 jela ni dogo mno, na badala yake, R Kelly anapaswa kutumia siku zake zote gerezanin kutokana na kuwaumiza watu wengi kwa miongo kadhaa.
–
Lizzette ameongeza kuwa, hafikirii unyanyasaji wa R Kelly kama utaisha kwa sababu kama waendesha mashtaka wa serikali walivyosema mtu huyo amethibitishwa mara kadhaa kuwa anatumia uwezo wake kupata kile anachotaka, na hawezi kupewa nafasi ya kuwaumiza wanawake tena.
–
Kwa upande Kitti Jones, mwingine kati ya waathiriwa wa R. Kelly, amesema kuwa hana tatizo na pendekezo la waendesha mashtaka, hata hivyo hakuna muda utakaompa yeye, na wengine, kurudisha wakati wao au kuondoa kiwewe chao kwenye mambo waliyopitia.
–
Wanawake wote wawili walionyeshwa katika makala ya “Surviving R. Kelly” ambayo yalizua mashtaka mapya, na hatimaye, kushindwa kwa Kelly na wanasema watakuwepo kwa hukumu yake baadaye mwezi huu.
–
Kama ilivyoripotiwa kuwa, Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani ilishinda hukumu dhidi ya Kelly Septemba 2021, na iliwasilisha tu mapendekezo yake ya kuhukumiwa kwake ikisema kuna orodha ya sababu za kumfunga kwa “zaidi ya miaka 25.”
–
Ikumbukwe kwamba, Kelly bado anakabiliwa na kesi nyingine ya serikali kutoka Illinois, pamoja na kesi ya serikali huko Minnesota.