Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemvua makamu wake Saulos Chilima mamlaka yote aliyokabidhiwa baada ya kutajwa katika kashfa ya ufisadi ya $150m (£123m) iliyohusisha kandarasi za serikali.
–
Ripoti ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (ACB) iliwataja maafisa 53 wa sasa na wa zamani kuwa walipokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara kutoka Uingereza na Malawi Zuneth Sattar kati ya 2017 na 2021, Alisema rais Chakwera
–
Maafisa waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na makamu wa rais na mkuu wa polisi ambaye amefutwa kazi.
–
“Kila bora ninachoweza kufanya kwa sasa, ambacho nimeamua kufanya, ni kunyima afisi yake majukumu yoyote aliyokabidhiwa huku nikisubiri ofisi ithibitishe madai dhidi yake,” Alisema Rais Chakwera katika hotuba ya kitaifa jana june 21, 2022.