ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, June 26, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Rais Tshisekedi asema Rwanda inaendesha “vita ya kiuchumi”

I am Krantz by I am Krantz
Jun 19, 2022
in HABARI
0
Rais Tshisekedi asema Rwanda inaendesha “vita ya kiuchumi”
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Tshisekedi ameituhumu Rwanda kuendesha vita ya kiuchumi na kujaribu kuinyakua ardhi ya Congo ili kujipatia rasimali kubwa ya madini.

Shirika la Habari la Associated Press limenukuu rais Tshisekedi  akisema hali ya usalama mashariki mwa Congo inaendelea kuzorota kwa sababu Rwanda inajaribu kudhibiti sehemu ya ardhi ya Congo yenye utajiri wa madini ya dhahabu na kobalti kwa manufaa yake.

RelatedPosts

Auto Draft

NBC Wanogesha hafla ya kukabidhiwa Kombe Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC j

Jun 26, 2022

ROSE REE AFUTE PICHA ZOTE ZA MCHUMBA WAKE

Jun 26, 2022

KAJALA ATOA AHAADI NZITO KWA HARMONIZE

Jun 26, 2022
Load More

Tshisekedi amesema kinachoendelea ni vita ya kiuchumi ya kuwania rasimali na Rwanda inayatumia magenge yake ya kigaidi.

Hapajawa na majibu yoyote kutoka nchini Rwanda kuhusiana na matamshi hayo ya Tshisekedi, ingawa Rwanda mara kadhaa imekanusha madai ya kuwaunga mkono waasi wa M23 ambao waliukamata mji muhimu mashiriki mwa Congo mapema wiki hii.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Kwenye matamshi yake rais Tshisekedi  amewataka viongozi wa kimataifa ikiwemo waziri mkuu wa Uingereza kuikosoa Rwanda bila kificho pindi watakapohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola baadae wiki ijayo mjini Kigali. “Raia wa mashariki mwa DRC hawana hatia lakini wanashambuliwa na jirani yetu” amesema Tshisekedi.

Matamshi ya kiongozi huyo huenda yatachochea moto kwenye mzozo unaotanuka baina ya mataifa hayo jirani ya eneo la maziwa makuu.

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Auto Draft
HABARI

NBC Wanogesha hafla ya kukabidhiwa Kombe Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC j

by I am Krantz
Jun 26, 2022
ROSE REE AFUTE PICHA ZOTE ZA  MCHUMBA WAKE
HABARI

ROSE REE AFUTE PICHA ZOTE ZA MCHUMBA WAKE

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
KAJALA ATOA AHAADI NZITO KWA HARMONIZE
HABARI

KAJALA ATOA AHAADI NZITO KWA HARMONIZE

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
HUYU NDIYO MWENYE WAFUASI WENGI ZAID TIKTOK
HABARI

HUYU NDIYO MWENYE WAFUASI WENGI ZAID TIKTOK

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
ALICHO KISEMA LUKAMBA KUHUSU HARMONIZE
HABARI

ALICHO KISEMA LUKAMBA KUHUSU HARMONIZE

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
CRDB BANK PAMOJA BONANZA ILIVYOFANA JIJINI DODOMA
BIASHARA

CRDB BANK PAMOJA BONANZA ILIVYOFANA JIJINI DODOMA

by I am Krantz
Jun 26, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In