Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino aipongeza klabu ya Yanga SC kutwaa Ubingwa wa Ligi kuu ya NBC msimu wa 2021/2022.
–
ADVERTISEMENT
Kupitia taarifa iliyotolewa na TFF leo Juni 27, 2022 imesema kwamba Infantino amesma ubingwa wa huo usingewezekana bila bidii ya timu nzima, ari na kujitolea.
Amesema kila mmoja kwenye klabu anapaswa kujivunia na ametoa pongezi kwa wote waliohusika katika mafanikio hayo.
–
ADVERTISEMENT
Aidha amemshukuru Rais wa TFF, Wallace Karia kwa mchango mkubwa anaoutoa katika maendeleo na ustawi wa soka la Tanzania na kanda ya Afrika Mashariki na Kati.