Mlinda Mlango wa klabu ya Yanga SC, Ramadhan Kabwili ameiaga timu yake leo Jumatatu, Juni 27, 2022 baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.
–
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema timu hiyo itabaki moyoni mwake siku zote kutokana na mambo mengi aliyojifunza akiwa klabuni hapo.

“Nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote wa miaka mitano niliotumikia Yanga nasema Asante na Mungu awabariki mtabaki kichwa mwangu daima.
–
“Nimejifunza mengi hasa kuamini kila nyakati za misimu bila kukata tamaa kunikomaza kwa hali zote za maisha yangu, leo najivunia kwa Watanzania, mashabiki, viongozi na wachezaji wenzangu mtabakia milele kichwani mwangu, Asanteni Wananchi” amendika Kabwili.