Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya amesafirishwa Alfajiri ya Leo Juni Mosi, 2022 kutoka Arusha kuelekea Mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kufunguliwa Kesi mpya.
ADVERTISEMENT
–
Sabaya amesafirishwa akitokea Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha Kwa kuwa yupo mahabusu kutokana na kukabiliwa na Mashtaka Mengine yasiyokuwa na dhamana.
–
Ikumbukwe kuwa siku ya Mei 31, 2022 Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliahirisha hukumu ya kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili na Wenzake sita Hadi Juni 10, 2022.
ADVERTISEMENT