Ameandika – Edvesta Safari
Simba na Yanga walichofanya siyo cha kiuungwana kwa upande wangu kwa afya ya soka letu. Nadhani busara ni bora kuliko mali. Nianze na Yanga ambayo imeachana na mchezaji wake Saido, huenda Saido ana makosa kweli ya kinidhamu km uongozi ulivyosema sawa sijakataa.
–
Lakini, najiuliza why kuachana nae hata kama amemaliza mkataba wake iwe ni sababu ya yeye kutoka kambini bila ruhusa?? Je, walikuwa wamemwambia akimaliza mkataba hawataendelea nae?? Na kama hawajafanya hivyo hawajamtendea haki. Hata kwa wale wanaofanya vibarua kwenye ofisi za watu ama taasisi unapewa nafasi ya kurenew contract ama unapewa wiki /siku / mwezi wa kujiandaa kisaikolojia n.k kisha unapewa rasmi barua ya ukomo wa kazi ? kibarua.
–
Yanga na Simba wakiwa na pesa wanajisahau sana kwa wachezaji na makocha wao. Bado ningali na Yanga kwanza, Yanga ilipokuwa haina pesa ilikuwa inawabembeleza wachezaji wake wacheze katika hali yeyote ile kuipa klabu matokeo chanya. Wamekuwa na pesa wanamwacha ghafla Saido.
–
Hivi mchezaji mwenye assist nyingi hivi na magoli ya kufunga unamwachaje kwa mfano kirahisi rahisi hivi?? Anyway uongozi unajua zaidi na una maamuzi yao. Lakini wangemwacha kijana wa watu walau afurahie ubingwa / mafanikio waliyosotea miaka mianne Yanga. Japo yeye sijasema kama ana miaka minne tangu asajiliwe Yanga. Nieleweke! Wakati mwingine maamuzi yanapofanyika, hebu tujaribu kuvaa viatu vya wengine katika maisha binafsi, familia, ndugu na jamaa inayomzunguka anayefanyiwa kabla ya kufanya hayo maamuzi.
–
Simba wameachana na Kocha wao, sioni kosa la kocha kuyumba kwa timu kwa muda mchache sana na kusahau mafanikio aliyoyawezesha kocha akiwa na timu. Tatizo kubwa la Simba siyo kocha bali ni wachezaji wenyewe (baada ya wachezaji muhimili kutokuwepo) na wengine majeruhi. Ikumbukwe mfano Cloutos Chama baada ya kuondoka pengo lake lilionekana, mashabiki walimtaka arudi, alirudishwa lakini fomular / combination ya uchazaji / wachezaji ilikuwa imeshasambaratika.
Haya leo hii ni sawa na Yanga walivyokuwa hawana pesa wakasajili wachezaji wasio na viwango vya ushindani, kocha Zahera pekee ndiye aliyeweza walau kupambana katika mazingira yale ya ukata na ukiipa klabu walau matumaini. Leo hii Simba imejisahau kwamba tatizo siyo kocha ni wachezaji, na Yanga imesahau pesa zinaisha itafikia wakati watawabembeleza wachezaji kucheza katika mazingira magumu wanaagana na Saido Ntibayokinza n.k Mashabiki wa Simba na Yanga hawana uvumilivu na, ni rahisi sana kusababisha uongozi na bodi kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuigharimu timu.
–
Nimalizie na Mtazamo wangu ; Uongozi wa Yanga wakimrudisha Bm3 nitashaa sana, Bm3 aliondoka Yanga kwa dharau sijapata kuona mchezaji aliyeondoka klabuni kwa dharau kama yeye kwa Tanzania. Natamani kuona Saido anacheza kati ya timu mbili hapa hapa Tanzania halafu akikutana na Yanga awafunge. Simba na Yanga wajitathimini wanapofanya maamuzi juu ya timu zao.