Klabu ya Simba kupitia kwa Meneja wa habari, Ahmed Ally imethibitisha kukwama katika mpango wa kumsajili winga wa klabu ya US Gendarmerie na Niger, Victorien Adebayor kufuatia kushindwana katika dau.
–
Adebayor (25) alikuwa midomoni mwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi baada ya kipaji chake wakati wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2021/22 kuwavutia wengi.
–
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally amesema: “Simba SC imeachana rasmi na dili la kumsajili Mshambuliaji wa Kimataifa wa Niger, Victorien Adebayor, na hii ni baada ya kushindwana kwenye upande wa dau analotaka yeye”