Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic, Kevin Wingfield (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera (Kulia) wakiwa wameketi kwenye madawati mawili kati ya madawati 200 yenye thamani ya TZS 25 milioni yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule za Sekondari za Lejico, Lufiyo na Mshewe mkoani Mbeya katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya hivi karibuni.Hii ni sehemu ya mpango wa benki wa Stanbic Madawati Initative unaoendelea ambao unakusudia kuchangia madawati kwa shule za Serikali mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifuatiwa na upandaji miti, ambao ni sehemu ya kampeni hiyo ukilenga kurejesha mfumo wa ikolojia kwa kupanda mti kwa kila dawati lililotolewa.