ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Sunday, June 26, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

TBS YATEKETEZA BIDHAA ZA VYAKULA NA VIPODOZI KATAVI

Shabani Rapwi by Shabani Rapwi
Jun 11, 2022
in HABARI
0
TBS YATEKETEZA BIDHAA ZA VYAKULA NA VIPODOZI KATAVI
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

RelatedPosts

Auto Draft

NBC Wanogesha hafla ya kukabidhiwa Kombe Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC j

Jun 26, 2022

ROSE REE AFUTE PICHA ZOTE ZA MCHUMBA WAKE

Jun 26, 2022

KAJALA ATOA AHAADI NZITO KWA HARMONIZE

Jun 26, 2022
Load More

BIDHAA mbalimbali za vyakula na vipodozi vyenye thamani takribani ya shilingi za Kitanzania milioni 7 zimeteketezwa katika dampo la Manispaa ya Mpanda baada ya kukutwa hazikidhi viwango kwa mujibu sheria ya Viwango Na 2 Sura 130.

 

–

 

Bidhaa hizo zilizoteketezwa mjini Mpanda ( 10/06/2022 )zilikamatwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Magharibi kwa ushirikiano na ofisi ya Kamanda Polisi, Katibu Tawala, Mamlaka ya Mapato na uongozi wa wilaya katika operesheni iliyofanyika Februari, Aprili na Mei, mwaka huu Mkoa wa Katavi katika Halmashauri zote za mkoa huo ambazo ni Manispaa ya Mpanda, Mlele, Mpimbwe, Tanganyika na Nsimbo.

 

–

 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuteketezwa kwa bidhaa hizo Kaimu Meneja TBS Kanda ya Magharibi, Rodney Alananga, alisema bidhaa hizo zilikamatwa maeneo ya mjini na vijijini katika maghala, maduka ya rejareja, jumla, supermarkets, masoko ya mipakani na stoo.

 

–

 

“Kati ya maeneo zaidi 100 yaliyokaguliwa, 36 yalikutwa na makosa kuuza au kuhifadhi bidhaa zilizokwisha muda, zenye viambata sumu, zisizosajiliwa na nyingi zinaingia nchini kwa njia zisizorasmi na mengine kukosa vibali vya kuuza au kusambaza vyakula na vipodozi toka TBS hivyo kuweza kuhatarisha afya na uchumi wa nchi,” alisema Alananga

 

–

 

Kwa mujibu wa Alananga, vipodozi vyenye viambata sumu vilivyopigwa marufuku zaidi ya aina 20 vilikamatwa ni pamoja na carolight, top lemon, clair men, diproson, Citrolight,carotene,Extra clair,clinic clear, betasol,prince clair, tent Claire, G&G na vingine.

 

–

 

ADVERTISEMENT

Alifafanua kwamba bidhaa hizo zikitumiwa zinaweza kuleta madhara ya kiafya kwa kusababisha magonjwa ya ngozi na Kansa:mfano kutoka mabaka au vipele sehemu mbalimbali za mwili na pia kuleta madhara ya mfumo wa uzazi au mzio wa ubongo wa watoto kwa mama wajawazito.

 

–

 

ADVERTISEMENT

“Vilevile vinaweza vikachangia kuleta Kansa ya ngozi na damu na hata kifo. Vilevile vyakula vilivyokamatwa ni vile vilivyokwisha muda wake wa matumizi ambavyo si chakula salama kutumiwa ambapo ilibidi kabla ya ukaguzi wa serikali wamiliki wanalazimika kujikagua, kutoa taarifa na kukabidhi hizo bidhaa kwa ofisi ya Afya na mazingira ya Halmashauri kwa ajili ya kuteketezwa kwa taratibu zilizopo.”

 

Alitaja bidhaa hizo kuwa ni kama vinywaji mbalimbali, sabuni, biscuits, Blue bands, hamira, viungo mbalimbali. “Havifai kwa matumizi sababu vinaweza leta madhara mbalimbali ya kiafya kama kuumwa tumbo na hata kansa,” alisema.   Alisema hatua zilizochukuliwa wakati wa operesheni ni kutaifisha bidhaa, kulipishwa tozo za uteketezaji ikiwemo gharama zote za usafirishaji, dampo na miundombinu na usimamizi wa uteketezaji.

 

–

 

Alananga alitoa wito kwa wafanyabiashara kuzingatia sheria na kutumia vizuri na kwa vitendo elimu na mafunzo wanayopata mara kwa mara kutoka TBS na wataalam wa mkoa na Halmashauri ili kushirikiana na serikali awamu ya sita katika kulinda afya za Watanzania na kukuza biashara kwa kuuza au kuingiza bidhaa bora na salama katika soko la Katavi.

 

–

 

Alisema ni muhimu wananchi kujenga tabia ya kusoma maelezo ya lebo katika bidhaa, kununua bidhaa za vyakula na vipodozi katika maduka yaliyotambuliwa na TBS, kudai risiti za manunuzi na kutembelea tovuti ya shirika kujua vipodozi na vyakula vilivyosajiliwa na kuthibitishwa.

 

–

 

Aidha, aliwataka wananchi na wafanyabiashara kutoa ushirikiano kwa TBS na vyombo vya dola hasa kutoa taarifa pale ambapo wanaona kuna wafanyabiashara wanakiuka taratibu hizi.

Related

ADVERTISEMENT
Shabani Rapwi

Shabani Rapwi

Shabani Rapwi (Kijana Mchapa Kazi) WhatsApp; 0689232546 Email ;shabanimohamed932@gmail.com

Related Posts

Auto Draft
HABARI

NBC Wanogesha hafla ya kukabidhiwa Kombe Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, klabu ya Yanga SC j

by I am Krantz
Jun 26, 2022
ROSE REE AFUTE PICHA ZOTE ZA  MCHUMBA WAKE
HABARI

ROSE REE AFUTE PICHA ZOTE ZA MCHUMBA WAKE

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
KAJALA ATOA AHAADI NZITO KWA HARMONIZE
HABARI

KAJALA ATOA AHAADI NZITO KWA HARMONIZE

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
HUYU NDIYO MWENYE WAFUASI WENGI ZAID TIKTOK
HABARI

HUYU NDIYO MWENYE WAFUASI WENGI ZAID TIKTOK

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
ALICHO KISEMA LUKAMBA KUHUSU HARMONIZE
HABARI

ALICHO KISEMA LUKAMBA KUHUSU HARMONIZE

by Shabani Rapwi
Jun 26, 2022
CRDB BANK PAMOJA BONANZA ILIVYOFANA JIJINI DODOMA
BIASHARA

CRDB BANK PAMOJA BONANZA ILIVYOFANA JIJINI DODOMA

by I am Krantz
Jun 26, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
June 2022
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930  
« May    
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In