
Inter wanashinikiza kumsajili Romelu Lukaku msimu huu wa joto. Lukaku pia anaitaka Inter, Mazungumzo yanaendelea kuhusu ada ya mkopo huku Lukaku akiwa tayari kupunguza mshahara wake.
–
Juventus wanakaribia kukamilisha usajili wa Paul Pogba . Mkataba unakaribia kukubaliwa, atapokea €8M + Nyongeza Kwa Mwaka. Juventus wanatarajia Pogba atasaini mkataba hivi karibuni.

Mazungumzo kati ya Manchester United na Barcelona juu ya uhamisho wa Frenkie De Jong huenda yakakwama kutokana na Mabosi wa Man Utd kuhofia kuwa Barca wanapanga bei kubwa kwa hali mbaya ya kiuchumi ya klabu hiyo.
–
Barcelona wanahitaji angalau kiasi kisichopungua €80m huku Manchester United wakisisitiza kuwa kiasi hicho ni kikubwa.
–
Tayari United wameanza mazungumzo na mchezaji Christian Eriksen kama mbadala wake endapo dili hilo litakwama.

Bayern wanakaribia kumsajili Sadio Mané, Makubaliano binafsi yatakubaliwa hivi karibuni, Ofa mpya itawasilishwa hivi hivi karibuni ili kupata makubaliano za pande zote mbili Liverpool na Bayern, mazungumzo yanaendelea.
–
ucas Torreira hataweza kurejea Fiorentina msimu ujao atarudi Arsenal. Lucas Alisema: “Nilitamani Kukaa Hapa Ila Kuna Mtu Hakutaka”. Fiorentina walikuwa na kipengele cha kumsajili kwa €15M Sawa na Tsh 36.4B lakini hawajakitumia kipengele hicho.
–
PSG inakaribia kumteua Christophe Galtier kama meneja wao mpya.
–
Mshambuliaji wa Everton Richarlison, 25, amekataa ofa ya kujiunga na Arsenal msimu huu – huku Chelsea na Tottenham Hotspur zikitajwa kama timu anazotaka kutua mbrazil huyo.