Southampton wamejaribu kuzuia nia ya Manchester City, Manchester United, Tottenham na West Ham kumnunua kiungo wa kati wa England, James Ward-Prowse, 27, kwa dau la pauni milioni 75.
–
Afisa mkuu mtendaji wa Bayern Munich Oliver Kahn anasema anatarajia fowadi wa Poland, Robert Lewandowski, 33, kusalia na mabingwa hao wa Ujerumani msimu huu wa joto.
–
Manchester City wapo kwenye mazungumzo ya juu zaidi ya kutaka kumsajili beki wa Brighton na Uhispania, Marc Cucurella, 23.
–
Ajax wanatazamiwa kuwasilisha ofa nyingine kwa winga wa Tottenham Hotspur na Uholanzi Steven Bergwijn, 24, lakini klabu hiyo ya Premier League haitakubali chochote chini ya pauni milioni 25.
–
Leeds United wanatazamia kumsajili winga wa PSV Eindhoven wa Uholanzi, Cody Gakpo, 23, msimu huu wa joto kama mbadala wa fowadi wa Brazil Raphinha, 25, ambaye analengwa na Arsenal.
–
Leeds wanamthamini Raphinha kwa pauni milioni 65 huku Tottenham, Chelsea na Barcelona pia wakimtaka.
–
Chelsea inamngoja mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Inter Milan kabla ya kushughulikia nia yao ya kumnunua fowadi wa Manchester City na Uingereza Raheem Sterling, 27.
–
Kipa wa Ujerumani Loris Karius, 29, yuko tayari kwa changamoto mpya anapotafuta klabu mpya ambayo huenda kuondoka kwake Liverpool kukiribia.
–
Kiungo wa kati wa Reims na Zimbabwe Marshall Munetsi, 26 anaweza kuletwa na Brighton kuchukua nafasi ya Yves Bissouma, kiungo wa kati wa Mali aliihama klabu hiyo na kuelekea Tottenham