Klabu kubwa Ulaya zinaamini kuwa Raheem Sterling, 27, yuko tayari kuondoka katika Manchester City msimu huu, huku Chelsea ikiwa ni miongoni mwa klabu zinazomtaka.
–
Paris St-Germain wamewasiliana na Lille kuhusu kusaini mkataba na Sven Botman baada ya mazungumzo na AC Milan kukwama ingawa Tottenham, Manchester United na Chelsea pia wameulizia kuhusu mlinzi huyo Mholanzi , 22, huku Newcastle wakiwa bado wanania naye.
–
Liverpool imefikia makubaliano ya sheria binafsi na mshambuliaji wa Benfica mwenye umri wa miaka 22, Darwin Nunez kwa ya kumsajili kama mbadala wa Sadio Mnane ambaye anahusishwa kutakiwa na Bayern Munich.
–
Barcelona wamekuwa katika mazungumzo kumuhusu mchezaji wa Manchester City Bernardo Silva lakini wanaweza kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 27, iwapo watamuuza kiungo wao rai wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25.
–
Kiungo wa kati wa Manchester City, Mjerumani Ilkay Gundogan, mwneye umri wa miaka 31 ambaye mkataba wake unaendelea hadi 2023, anatakiwa na Barcelona na Juventus.
–
Oleksandr Zinchenko yuko tayari kuondoka Manchester City msimu huu, lakini klabu zozote zenye nia na yeye ambazo ni pamoja na Wolves, Arsenal, Everton, Leicester na West Ham, zitapaswa kumhakikishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwamba zita mpatia muda wa mechi katikati ya uwanja, ambapo mchezaji huyo anayetumia guu la kushoto zaidi hucheza kwa ajili ya Ukraine.
–
Fenerbahce wameelezea nia yao kwa mchezaji wa Manchester United, Andreas Pereira lakini mashetani hao wekundu pia wamemwambia kiungo wa kati Mbrazil mwenye umri wa miaka 26 kuwa atapewa fursa ya kumvutia meneja mpya Erik ten Hag kabla ya msimu kuanza.
–
Leeds United na Aston Villa wameanza mazungumzo na mshambuliaji Muingereza mwenye umri wa miaka 18 Sonny Perkins, ambaye ameonekana kwatika kikosi cha kwanza mara tatu katika klabu ya West Ham.
–
Wolves wamemthamanisha kiungo wa kati Muingereza Morgan Gibbs-White, mwenye umri wa miaka 22, kwa thamani ya pauni milioni 25 ambaye amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia katika klabu za Nottingham Forest na Southampton baada ya kumalizika kwa msimu wa mkataba wake wa mkopo katika Sheffield United.