Paul Pogba bado hajakamilisha mkataba wake wa uhamisho huru wa kutoka Man United kuelekea Juventus huku kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29, akisubiri kuona iwapo Zinedine Zidane anateuliwa kama kocha wa Paris St-Germain.
–
PSG wanajaribu kumshawishi kocha wa zamani wa Real Madrid Zidane, 49, kuchukua nafasi ya Mauricio Pochettino kama meneja wao mpya.
–
Arsenal wako tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 42 kwa ajili ya kiungo wa kati wa Lazio Mserbia Sergej Milinkovic-Savic, ingawa Newcastle wanaweza pia kuweza dau kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17.
–
Sevilla inasema kiungo wa safu ya kati-nyuma Mfaransa Jules Kounde anaangalia uwezekano wa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu, huku Chelsea ikitarajiwa kusaini mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
–
Klabu mpya iliyopandishwa daraja nchini Uingereza ya Nottingham Forest inamlenga kiungo wa kati wa Arsenal Muingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, ambaye amekuwa akicheza kwa mkataba wa mkopo katika Roma msimu uliopita.
–
Tottenham wameafiki mkataba wa kumnunua mchezaji wa Middlesbroug Djed Spence, ambaye amekuwa akichea kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Forest msimu uliopita, huku gharama ya kiungo huyo wa nyuma-kulia mwenye umri wa miaka 21, rai awa Uingereza akifahamika kulipwa karibu pauni 20.
–
Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale anasema kuwa atajiunga na Getafe baada ya kuondoka Real Madrid msimu hu una mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 atafanya uamuzi juu ya hali yake ya baadaye baada ya mwisho wa Ligi ya nchi yake