West Ham wanatazamiwa kutoa takriban pauni milioni 30 kwa mshambuliaji wa Chelsea, Armando Broja, 20, ambaye alicheza kwa mkopo Southampton msimu uliopita.
–
Arsenal wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Brazil Raphinha kutoka Leeds United, huku nia ya Barcelona kumnunua mchezaji huyo wa miaka 25 ikiwa imepungua.
–
Tottenham waliwasiliana na kambi ya mchezaji wa Denmark Christian Eriksen wiki chache zilizopita lakini hawajafuatilia nia ya mchezaji wao wa zamani mwenye umri wa miaka 30, ambaye alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita huko Brentford.
–
Manchester United imekuwa na ofa ya pauni milioni 55 kwa mshambuliaji wa Brazil, Evanilson iliyokataliwa na Porto lakini klabu hiyo ya Old Trafford inapanga kutoa ofa mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola anasema anataka kiungo wa kati wa Ureno, Bernardo Silva, 27, ambaye amekuwa akihusishwa na Barcelona, kusalia na mabingwa hao wa EPL lakini akaongeza kuwa hapendi kuwaweka wachezaji “wasio na furaha” katika klabu hiyo.
–
Kocha wa Nottingham Forest Steve Cooper, ambaye alikiongoza kikosi chake kupanda EPL msimu uliopita, yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo.
–
Kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojberg amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Tottenham lakini Spurs hawana nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
–
Baada ya kushindwa kumsajili mlinzi Mholanzi, Jurrien Timber mwenye umri wa miaka 21, Manchester United inaweza kuchukua hatua ya kumsajili mchezaji mwenzake wa Ajax, Lisandro Martinez. Beki huyo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 pia analengwa na Arsenal.