ADVERTISEMENT
Tottenham inataka kumsajili mshambuliaji wa Brazil Richarlison 25, na wing awa Uingereza Anthony Gordon , 21 kutoka Everton katika mikataba miwili. Chelsea pia imeonesha nia ya kutaka ya saini ya Richarlison.
–
Lakini Everton haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Goodison Park inakamilika 2025.
–
Spurs wanapigiwa upatu kumsajili beki wa Barcelona na Ufaransa, Clement Lenglet, licha ya Roma kuwa nahamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.

Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 18, atakuwa mchezaji anayesakwa sana na Real Madrid msimu ujao , lkicha ya kwamba klabu hiyo ya Uhispania inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea na Liverpool.
–
Mshambuliaji wa Liverpool na Misri Mohamed Salah, 30, anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu wa 2022-23 akiwa mchezaji huru. Salah amefunga magoli 156 katika mechi 254 tangu alipojiunga na Reds mwaka 2017.
–
Arsenal wamewasilisha ofa ya pauni milioni 35 kwa mlinzi wa Ajax, Lisandro Martinez na wanaonekana kuiongoza Manchester United katika kinyang’anyiro cha kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 24.
–
Manchester United wanatumai kuhitimisha kandarasi za kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong, 25, na kiungo wa kati wa Denmark, Christian Eriksen, 30, na kisha wataelekeza umakini wao kumsaka mshambuliaji, huku Mbrazil wa Ajax, Antony, 22, akiwa lengo lao kuu.

Newcastle United wanatazamia kukamilisha usajili wa pauni milioni 32 wa mlinzi wa Lille Mholanzi, Sven Botman, 22, lakini wako tayari kuendelea na harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Reims Mfaransa, Hugo Ekitike, 20.
–
Mfaransa Christophe Galtier, ambaye aliiongoza Nice msimu uliopita, anakaribia kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Paris St-Germain, huku Mauricio Pochettino akikaribia kuondoka katika klabu hiyo licha ya kushinda taji la ligi.
–
Barcelona hawataboresha ofa yao ya kandarasi kwa mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele, ambaye mkataba wake na timu hiyo ya La Liga unamalizika tarehe 30 Juni. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia ana ofa kutoka kwa Bayern Munich, Chelsea na PSG. Dembele anatazamiwa kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake katika saa 72 zijazo.
ADVERTISEMENT