Liverpool wanamfuatilia mshambuliaji wa Rennes, Mfaransa Martin Terrier, 25, kama mbadala wa Sadio Mane, iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal, 30, ataondoka Anfield.
–
Arsenal bado wanamtaka kiungo wa Leicester, Youri Tielemans huku Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 25 akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto, lakini vilabu vingine viwili pia viko kwenye kinyang’anyiro hicho.
–
West Ham wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsajili beki wa Rennes, Nayef Aguerd. The Hammers pia walijaribu kumsajili mchezaji huyo wa Morocco mwenye umri wa miaka 26 msimu uliopita wa joto.
Inter Milan wanatarajiwa kufanya mazungumzo na mwanasheria wa mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku, 29, kuangalia namna mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anavyoweza kurejea Serie A.
–
Leeds United wanakabiliwa na vita ya fedha ya pauni milioni 10 dhdi ya klabu ya Bundesliga, Borussia Dortmund ili kumsajili beki wa kulia wa kimataifa wa Denmark, Rasmus Kristensen, 24, kutoka Red Bull Salzburg.
Barcelona wamemuweka sokoni kwa mkopo mlinzi wa kimataifa wa Ufaransa, Clement Lenglet, 26, huku vilabu kadhaa vya ligi kuu England bikionyesha nia ya kumtaka.
–
Liverpool wanajiandaa kuipiku Leeds katika kumsajili beki wa Scotland, Calvin Ramsay mwenye umri wa miaka 18 kutoka Aberdeen.
–
Manchester United wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na England, Mason Mount, 23, ambaye bado hajasaini mkataba mpya Stamford Bridge.
–
Meneja wa Barcelona Xavi amefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, kuangalia uwezekano wa kumsajili.
–
Beki wa kushoto wa Manchester City wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, anavivutiwa vilabu vya Everton na Newcastle.