Klabu ya Inter Milan ya Italia imekubali dili la kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Chelsea.
–
The Blues walimsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Inter kwa pauni milioni 97.5 mnamo Agosti 2021, lakini atarejea katika kikosi hicho cha Serie A ambacho kilikuwa na matatizo msimu uliopita.
–
Ada ya mkopo kwa Lukaku ni takriban euro 8m (£6.9m). Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alifunga mabao 15 katika michuano yote msimu uliopita akiwa na Chelsea, na mabao manane katika mechi 26 za Premier League.
Mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski bado anataka kuondoka Bayern Munich, licha ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Ujerumani, Hasan Salihamidzic kusafiri kukutana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ana kwa ana kujaribu kumshawishi kuendelea kusalia klabuni hapo.
–
Real Madrid wameongeza nia ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Uingereza, Raheem Sterling katika wiki za hivi karibuni, huku Barcelona na Chelsea wakifuatilia maendeleo kuhusu mustakabali usio na uhakika wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 katika klabu ya Manchester City.
–
Barcelona wanataka kumsajili beki wa Ufaransa, Jules Kounde, lakini hawataki kulipa euro milioni 60 za Sevilla (£51.5m) kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
–
Arsenal na Newcastle wanamtaka kiungo wa kati wa Uhispania Fabian Ruiz, 26, ambaye mkataba wake na Napoli utakamilika 2023.
–
Tottenham wanatazamia kufanya mazungumzo zaidi ya kumsajili beki wa kulia wa timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21, Djed Spence kutoka Middlesbrough. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikaa msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Nottingham Forest na kuwasaidia kupanda EPL.
–
Borussia Dortmund, ambayo ilimuuza mshambuliaji wa Norway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 21 kwa Manchester City, inatazamiwa kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast, Sebastien Haller kutoka Ajax kwa euro milioni 36.
–
Wolves wanatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Gabriel Barbosa, 25, kutoka Flamengo na kiungo wa kati wa Argentina, Enzo Fernandez, 21, kutoka River Plate.