Chelsea inakaribia kuafikiana na Leeds kuhusu dau la kumnunua mshambuliaji wa Brazil na Leeds United, Raphina mwenye umri wa miaka 25 , ambaye pia anazivutia klabu kama vile Arsenal na Barcelona.
–
Chelsea sasa imebadilisha mawazo yake na sasa inamnyatia beki wa Milan na Slovakia mwenye umri wa miaka 27, Milan Skriniar ambaye pia analengwa na PSG baada ya kubaini kwamba kifungu cha kumuuza mchezaji wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 22 ni ghali mno.

PSG imekubaliana masharti na Skriniar Pamoja na kiungo wa kati wa Lille na Ureno Renato Sanchez 24 na mshambuliaji wa Itali mwenye umri wa miaka 23 Gianluca Scamacca, ambaye anaichezea Sassuolo. Mabingwa hao wa Ufaransa sasa watalazimika kuweka makubaliano na klabu hizo tatu.
–
Chelsea imehusishwa na harakati za kumnunua mchezaji mwengine wa tatu wa klabu ya Manchester City. The Blues inataka kumnunua mshambuliaji wa Ukraine international Oleksandr Zinchenko, 25, kutoka kwa mabingwa hao wa ligi ya Premia baada ya kuanzisha mazunumzo ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 27, kutoka kwao mbali na kuhusishwa na usajili wa beki wa Uholanzi Nathan Ake, 27.

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anatumai kumsaini kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong ,25, kutamshawishi kiungo mchezeshaji wa Denmark Christian Eriksen ,30, kujiunga na klabu hiyo ya Old Trafford.
–
Tottenham wameimarisha harakati zao za kutaka kumsaini mshambuliaji wa Everton na Brazil Richarlison , 25 lakini ombi la £20m ambalo lilishirikisha winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 24, limekataliwa na the Toffees.
–
Middlesbrough imakasirishwa na hatua ya klabu ya Tottenham kusitoisha mkaubaliano ya kumnunua beki wa kulia wa Englandanayechezea timu ya umri wa chini ya miaka 21 Djed Spence na hilo linaweza kufungua milango ya Nottingham Forest kumnunua mchezaji wa miaka 21 , ambaye aliisaidia klabu hiyo ya City Ground kupandishwa hadhi ya kucheza katika ligi ya Premia msimu uliopita.
–
Crystal Palace inakaribia kumsaini kungo wa kati wa Lens Cheick Doucoure katika makubaliano yenye thamani ya Yuro Milioni 21 pamoja na marupurupu kwa mchezaji huyo wa Mali mwenye umri wa miaka 21.
–
Fulham imeruhusiwa kuzungumza na kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira baada ya kukubaliana da una Manchester United ,ijapokuwa mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 26 anataka kusalia katika timu ya Flamengo ya Brazil ambapo yupo kwa mkopo.

Southampton imejiunga na klabu nyneginezo baada ya kuvutiwa na kiungo wa kati wa Burnley na England Josh Brownhill 26.
–
Manchester City imekubali kumuuza mchezaji wa England anayechezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19 Sam Edozie , 19, kwa klabu ya Ujerumani Bayer Leverkusen kwa dau la £10m.