Kiungo wa Denmark, Christian Eriksen, 30, ameamua kutafuta changamoto mpya na anajiandaa kutimka Brentford. Vilabu vya TottenhamHotspur na Manchester United vinammendea nyota huyo.
–
Juventus wana uhakika na matumaimi makubwa ya kumsajili Paul Pogba, 29 bure kutoka Manchester United. Kiungo huyo mfaransa amekubali kusaini mkataba wa miaka minne.
–
Nyota wa Tottenham Steven Bergwijn anasema anasakwa na vilabu kadhaa wakati huu ambapo winga huyo wa Uholanzi, 24, akitaka kutimka, Ajax wako kwenye mazungumzo kwa ajili ua kumsajili msimu huu.
–
Kama mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 23, ataondoka Sevilla na kujiunga na Chelsea, basi Barcelona itaelekeza nguvu zake kumsajili Kalidou Koulibaly, ingawa Napoli inaweza kutaka angalau £34.1m kwa ajili ya mlinzi huyo Msenegal.
–
Inter Milan inajiandaa kumsajili Paulo Dybala bure kutoka Juventus, huku mshambuliaji huyo muargentina mwenye miaka 28, anasaini mkataba wa miaka 3.
–
Klabu ya Argentina ya River Plate imewasiliana na mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez, 35 ili ajiunge bure anapomaliza mkataba na klabu ya Atletico Madrid msimu huu.
–
Chelsea wanakaribia kumnasa kipa Mmarekani Gabriel Slonina, 18, kutoka Chicago Fire baada ofa ya Real Madrid ya £8.5m kukataliwa.
–
Leeds United wanaongoza katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa New York City mwenye miaka 23 muargentina Valentin Castellanos.
–
Manchester United wanamfukuzia pia winga wa Brazil Antony, 22, kutoka Ajax, na kiungo wa Uholanzo Frenkie de Jong, 25, kutoka Barcelona.