Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, yuko tayari kurejea katika Inter Milan kwa gharama ya mkopo wa £8.5m pamoja na marupurupu aliyokubaliwabaina ya klabu hizo.
–
Tottenham wana matumaini ya kuwapiku mahasimu wao wa kaskazini mwa London Arsenal katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa Manchester City Mbrazili Gabriel Jesus.
–
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kufanya dai jipya kwa ajili ya kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi mwenye umri wa miaka 25 Frenkie de Jong.
–
Mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 27, amekuwa akiwauliza watu kuhusu maisha katika magharibi mwa London huku klabu ya Chelsea ikiwa na nia naye.
–
Kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, yuko katika orordha ya Manchester United ya wachezaji inayoweza kusaini mkataba nao iwapo watashindwa kusaini mkataba na De Jong.