Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe amefunguka na
kuweka wazi nia yake ya kuutaka tena Urais katika uchaguzi Mku ujao wa 2025 kwa kusema kuwa atamuunga mkono Rais Samia hasa ukizingatia kuwa amejitahidi sana kuongoza nchi.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uanachama na Katibu wa uenezi Shaka Hamdu Shaka kama mwanachama hai wa CCM kwa mara nyingine, Membe amesema kuwa ameamua kutoa msimamo huo mapema ili asije kunukuliwa tofauti.
“Uchaguzi 2025 ni mama, natoa msimamo mapema kabisa na hii ni kutoka ndani ya moyo wangu, naomba ieleweke kuwa mama amejitahidi sana ni lazima tumpe nafasi, mimi na muunga mkono” Benard Membe.
Membe alieleza pia jinsi alivyofarijika kupokelewa tena ndani ya chama huku akisema alikuwa akiona urafiki na mioyo iliyajaa furaha kwenye Kamati Kuu tofauti na alivyotegemea.
Aliongeza kusema kuwa yupo tayari kusaidia shughuli zote za chama ikiwa ni pamoja na kushauri pale ambapo anahitajika kufanya hivyo.