Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA) imekamata marobota ya vitenge 507 yaliyoingizwa nchini kinyume cha sheria.
–
Marobota hayo yameingizwa nchini na Mfanyabiashara raia wa China kwa njia za magendo kupitia Kampuni yake inayoitwa Kapansky Company Limited.
ADVERTISEMENT
Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Robert Manyama (kushoto) akioneshwa marobota ya vitenge yaliyokamatwa na TRA yakiwa yameingizwa nchini na Mfanyabiashara raia wa China kwa njia za magendo kupitia Kampuni yake inayoitwa Kapansky Company Limited na kuhifadhi mzigo huo kwenye Ghala la Kampuni ya Shinyanga Emporium lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ukiwa hauna nyaraka zozote za forodha. Kushoto ni Meneja wa Idara ya Ukaguzi wa Kodi kutoka TRA Bw. Deogratius Shilima.
ADVERTISEMENT
Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Robert Manyama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya kukamatwa jumla ya marobota 507 ya vitenge yaliyoingizwa nchini na Mfanyabiashara raia wa China kwa njia za magendo kupitia Kampuni yake inayoitwa Kapansky Company Limited na kuhifadhi mzigo huo kwenye Ghala la Kampuni ya Shinyanga Emporium lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ukiwa hauna nyaraka zozote za forodha.
Marobota ya vitenge yaliyokamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yakiwa yameingizwa nchini na Mfanyabiashara raia wa China kwa njia za magendo kupitia Kampuni yake inayoitwa Kapansky Company Limited na kuhifadhi mzigo huo kwenye Ghala la Kampuni ya Shinyanga Emporium lililopo Vingunguti jijini Dar es Salaam ukiwa hauna nyaraka zozote za forodha.