Akitoa Hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Richard Kabate amesema, mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao na kila mmoja atatumikia kifungo cha miezi sita jela.
Mbali na adhabu hiyo mshtakiwa kwa kwanza ambaye ni Seif atakapomaliza kutumikia kifungo chake atatakiwa kuilipa CWT fidia zaidi ya shilingi milioni 7.5 na mshtakiwa wa pili ambaye ni Allawi atakapomaliza kutumikia kifungo chake atatakiwa kuilipa CWT shilingi milioni 6.2.
Awali jopo la mawakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambanna na Rushwa Nchini (TAKUKURU) liliiomba mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa adhabu kali kwa washtakiwa hao.