Mtandao wa Netflix upo kwenye mchakato wa kuanza kutafuta washiriki wa kipindi cha TV ambacho maudhui yake yametokana na filamu maarufu ya ‘Squid Game’ ya Korea Kusini.
–
Lakini katika kipindi hiki cha Netflix hakutakua na hatari yoyote itakayopelekea kifo kwa mshiriki kama ilivyokuwa katika filamu ya ‘Squid Game’ ambapo washiriki walishindana na kuuana wenyewe kwa wenyewe.
–
Mchezo huu utahusisha washiriki 456 kutoka nchi mbalimbali duniani, atakayeshindwa atarudi nyumbani mikono mitupu na mshindi atapewa kiasi cha dola milioni 4.56 sawa na Tsh bilioni 10.
–
Mshiriki lazima awe na umri kuanzia miaka 21, ajue kuongea kiingereza na awe na muda wa wiki 4 kwa ajili ya kushiriki katika kipindi hicho.