West Ham wamekamilisha uhamisho wa kudumu wa mlinda mlango wa Paris Saint-Germain, Alphonse Areola kwa kandarasi ya miaka mitano.
–
Areola alijiunga kwa mkopo msimu uliopita wa joto huku West Ham wakiwa na chaguo la kununua, moja kwa moja baada ya muda wake wa mkopo kumalizika.
–
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anajiunga na West Ham kwa mkataba wa miaka mitano hadi msimu wa joto wa 2027, na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.
–
“Ninajisikia vizuri, kusaini mkataba wa kudumu na nina furaha kubaki hapa. Lazima nifanye kazi yangu na kufanya kila kitu ili kuwafanya mashabiki wawe na furaha” Areola alisema