Waziri wa Nishati, January Makamba, ameliomba Bunge kumuidhinishia Bajeti ya jumla ya Shilingi 2,905,981,533,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake.
–
Shilingi 2,676,229,576,000 sawa na asilimia 99 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, kati ya fedha hizo, Shilingi 2,508,756,128,000 ni fedha za ndani na Shilingi 167,473,448,000 ni fedha za nje.
–
Shilingi 29,751,957,000 sawa na asilimia 1 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida, kati ya fedha hizo Shilingi 15,025,821,000 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 14,726,136,000 kwa ajili ya Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.