Ni mara ya pili katika historia kwa timu zinazoshiriki ligi kuu nchini Tanzania kutwaa ubingwa bila kupoteza(unbeaten) Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 2009/2010 Mnyama Simba alivyotwaa ubingwa bila kupoteza chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri ambapo mnamo April 21,2010 katika uwanja wa Taifa( kwasasa Benjamin Mkapa) baada ya mchezo wao wa mwisho dhidi Mtibwa Sugar kutoka Manungu Morogoro.
–
Miongoni mwa mastaa waliotwaa ubingwa msimu huo ni pamoja na akina Mussa Hassan Mgosi,Mohamedi Banka, Nico Nyagawa,Juma Jabu,Joseph Owino,Kelvin Yondani,Juma Nyoso, Uhuru Selemani na Salum Kanoni. Wengine ni Juma Kaseja,Deo Munish,Ally Mustafa,Jabir Azizi Haruna Shamte na Amri Kiemba. Simba ilicheza mechi 22,walishinda 20 na kutoa sare mechi mbili wakivuna alama 62 wakifunga magoli 50 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 12. katika sare walizopata ni kutoka kwa African Lyon na Kagera Sugar.
–
Ikumbukwe pia Simba wakati huo ilikaa miaka miwili mfululizo bila kombe hilo ambalo kwa muda wote huo lilikuwa kwa watani zao Yanga. Nafasi ya tatu katika msimu huo ilichukuwa na Azam FC. Msimu wa 2021/2022.

Ni msimu mzuri kwa Yanga,msimu ambao nao wametengeneza historia baada ya Simba kufanya hivyo miaka 12 iliyopita. Yanga imenyanyua makwapa bila kupoteza na sasa wana kila sababu ya kutamba mbele ya watani zao Simba kwamba wamevunja historia.
Katika michezo 29 waliocheza wameshinda mechi 29 walizocheza wamebeba alama 71 ambazo hakuna timu inayoweza kuzifikia. Simba kupitia meneja wake wa habari na Mawasiliano Ahmed Ally waliwapongeza watani wao wa jadi kwa kubeba ubingwa baada ya miaka minne kupita.
Na kwasasa kinachosubiriwa na mashabiki wengi ni ukarabati wa vikosi vya wanakariakoo ambavyo vinamashabiki ndani na nje ya Tanzania. Kadhalika mashabiki wake wanatamani kuona vikosi hivyo vitafanya nini katika mashindano ya kimataifa ambayo wote watashiriki.
–
Ameandika , Na, Adamu Hussein Chauya