Serikali imesema zaidi ya Malori 40 ya usafirishaji wa mazao yanayoenda Nchi jirani yamekwama mpakani Namanga kwa sababu zinazodaiwa kuwa kukosa kibali cha kusafirishia mazao
–
Akizungumza jijini Dodoma Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema sababu kubwa zilizopelekea malori hayo kukwama mpakani hapo Namanga ni kutokana na wafanyabiashara wa mazao mbalimbali kushindwa kuomba kibali cha usafirishaji ambapo vibali hivyo kwa sasa vitapatika kwa kupitia maombi ya njia ya mtandao
–
Aidha Mhe. Bashe amewataka wafanyabiashara wa mazao kuacha kufanya safari ya kusafirisha mazao bila ya kupata kibali cha kusafirisha mazao hayo nje ya Nchi pamoja na kibali cha ukaguzi wa afya ya mimea.
–
“Tumetoa tangazo tumeliweka katika online lakini watu nadhani hawakuelewa na sasa nimeamua niseme tukikukamata unavuka mpaka bila ya export licence tutaikamata hiyo mali na kukuchukulia hatua za kisheria” amesema Waziri Bashe