Waziri wa Utalii na mambo ya kale visiwa vya Zanzibar ametoa onyo dhidi ya watu wanaotukana watalii kisa mavazi yao
–
Waziri Simai Mohammed ameiambia BBC kwamba serikali itachukua hatua kwa watu wanaowaudhi watalii, ambao ni muhimu kwa uchumi wa visiwa hivyo.
–
“Tabia hii ya kuwatukana wageni inapaswa kukomeshwa”
–
“Katika baadhi ya maeneo ya Mji Mkongwe, [idadi] ya matukio hayo yamekuwa ya mengi sana. Yeyote anayewatukana watalii, nitamshughulikia kwa uzito mkubwa,” alisema.
–
Utalii ni chanzo kikubwa cha mapato kwenye visiwa hivyo na ndio chanzo chake kikubwa cha fedha za kigeni.