KANUNI HIZI ZITAKUSAIDIA
KANUNI HIZI ZITAKUSAIDIA
1. Jifunze kuweka akiba.
2. Jiepushe na vikao vya masengenyo vitakuongezea nguvu hasi.
3. kaa na waliofanikiwa, jifunze kutoka kwao.
4. Usiishie kupanga tu, fanya kwa vitendo.
5. Kuwa mstaarabu na mwema kwa watu.
6. Usipoteze muda, hakikisha unafanya jambo la maana muda wote.
7. Usikae na kinyongo na visasi, muwajibishe mtu inavyostahili.
8. Usiruhusu watu wakuzoee sana, watakuona hauna maana, watu ndio mtaji wako wa kwanza.
9. Fikiria sana mustakabali wa maisha yako wa miaka mitano sita baadae.
10. kila siku jifunze kitu kipya hasa vile ambavyo dunia haiwezi kuviepuka, jifunze mambo makubwa na nyeti yanayoendesha dunia.
11. Ukifanikiwa, wafundishe na wengine. Wasaidie pia.
12. Jali sana afya yako ya kimwili na kiroho maana bila hivyo huwezi kufanya chochote.
13. USIOGOPE!