Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja limethibitisha kufariki dunia kwa mtu mmoja aitawe Shaaban Mkubwa Mwinjaa mwenye umri wa miaka 33 baada ya kunasa katika nyaya za umeme kwenye kuta za kiwanda cha matofali kilichopo Masingini.
–
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdalla Hussein Mussa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari huko ofisini kwake Mwembemadema Mjini Unguja
Kamanda Mussa Amesema mtu huyo alikimbia baada ya kumgonga mpanda baisekeli aitwae majid Charles Jumma ambae alikua akivuka barabara.
–
Aidha amesema mbali na tukio hilo katika kipindi cha wiki moja kutoka Juni 24 hadi 30 mwaka huu amesema jumla ya watuhumiwa kumi wamekamatwa kwa makossa mbalimbali