Mfanyakazi wa Benki ya NMB mkoani Mtwara,, Simon Jogwe ni miongoni mwa wazazi waliopoteza watoto katika ajali ya gari iliyotokea leo Kata ya Magegeni, Manispaa ya Mtwara Mikindani.
–
Jogwe amepoteza watoto wa pekee wawili Johari Simon miaka 7 na Emmanuel Simon miaka 5, ambao wote walikuwa ni wanafunzi wa shule ya msingi King David.
–
Ajali hiyo iliyohusisha gari la shule hiyo (King David Primary School) imeua watu 10, wakiwemo wanafunzi nane, dereva na mama mmoja ambaye aliomba lift katika gari hiyo.
–
Kwa mujibu taarifa ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Hamad Nyembea, wanafunzi watano wasichana na watatu wavulana ndiyo waliopoteza maisha.