Klabu ya Azam FC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji kutoka Nigeria, Isah Ndala, kwa mkataba wa miaka miwili.
–
Ndala alikuwa akichezea Plateau ya Nigeria, amesaini mkataba mbele ya mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin Mbali na kucheza Plateau, Ndalla amepita pia katika timu ya Sevan ya Armenia na Nasarawa United ya Nigeria.
Huo unakuwa ni usajili wetu wa tatu kwa klabu ya Azam FC kuelekea msimu ujao, baada ya jana kuwatangaza nyota wawili kutoka Ivory Coast, Kipre Junior na Tape Edinho.