ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, August 8, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki Ya CRDB Na IFC Kuongeza Upatikanaji Wa Mitaji Kwa Wajasiriamali Nchini Tanzania Na Burundi

I am Krantz by I am Krantz
Jul 12, 2022
in BIASHARA, HABARI
0
Benki Ya CRDB Na IFC Kuongeza Upatikanaji Wa Mitaji Kwa Wajasiriamali Nchini Tanzania Na Burundi
0
SHARES
33
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Afrika, Sergio Pimenta (kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 105 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo katika hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam.

 

========   =======    ========

RelatedPosts

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

Aug 2, 2022

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEZESHAJI KUTOKA BENKI YA CRDB

Jul 21, 2022

BENKI YA CRDB KATIKA MAONESHO YA 46 YA SABASABA

Jul 3, 2022
Load More

 

Benki ya CRDB na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) leo wameingia mkataba wa uwezeshaji utakaongeza upatikanaji wa fedha kwa wajasiriamali wadogo na wakati nchini Tanzania na Burundi, na kusaidia kuimarisha uchumi wa nchi zote mbili kutokana na athari za janga la UVIKO-19. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Johari Rotana iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi waaandamizi wa taasisi hizo.

Chini ya ushirikiano huo, IFC inatoa mkopo wa dola milioni 100 kwa Benki ya CRDB Tanzania, nusu ya fedha hizo zitakuwa kwa shilingi ya kitanzania, na mkopo wa dola milioni 5 kwa Benki ya CRDB Burundi kusaidia mikopo kwa wafanyabiashara wadogo katika nchi zote mbili, hasa kwa wafanyabiashara wanaomilikiwa na wanawake.

Katika mkataba huo, asilimia 25 ya mkopo unaoelekezwa nchini Tanzania utatolewa kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake. Imebainishwa kuwa fedha hizo zitaongeza upatikanaji wa mikopo ya muda mrefu, ambayo imekuwa adimu kupatikana tangu kuzuka kwa janga la COVID-19.

Mikopo hiyo ni sehemu ya mpango wa IFC wa uwezeshaji wa tabaka la chini katika uchumi, ambao unalenga kusaidia taasisi za kifedha kutoa mikopo kwa wajasiriamali na wafanyabisahara wadogo ambao wameathiriwa zaidi na janga la UVIKO-19. Ufadhili wa IFC pia unasaidiwa na Dirisha la Sekta ya Binafsi la Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa.

Wajasiriamali ni kundi muhimu kwa uchumi wa Tanzania na Burundi. Nchini Tanzania, wastani wa biashara ndogo ndogo na za kati ni milioni 3.2, huchangia asilimia 27 ya Pato la Taifa, na kuajiri zaidi ya watu milioni 5. Hata hivyo, takriban asilimia 81 ya biashara hizi hazina uwezo wa kupata fedha. Biashara nchini Burundi pia zinachangamoto kubwa katika kupata fedha.

“Fedha hizi zimekuja wakati muafaka na zitaongeza uwezo wetu wa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati huku tukisaidia kuongeza usawa wa kijinsia katika mnyororo wa thamani. Benki ya CRDB tunaamini kuwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake ni msingi wa maendeleo. Wanawake wameathirika kwa kiasi kikubwa sana janga la UVIKO-19, ambalo limepelekea changamoto nyingi za kiuchumina kuathiri moja kwa moja maisha ya familia na jamii zao,” alisema Abdulmajid Nsekela Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB wakati wa hafla ya utiaji sahihi.

Nsekela aliongezea kuwa ufadhili wa IFC utasaidia maendeleo ya sekta mbalimbali za maendeleo nchini, ikiwamo biashara, kilimo, afya, elimu, makazi, na miundombinu. Maeneo mengine ni pamoja na miradi inayozingatia mabadiliko ya tabianchi, wajasiriamali, pamoja na biashara zinazomilikiwa na wanawake kama ambavyo imesisitizwa katika mkataba huo wa ushirikiano baina ya Benki ya CRDB na IFC.

“Ushirikiano kati ya IFC na Benki ya CRDB utasaidia ukuaji wa sekta ya ujasiriamali katika nchi hizi ambapo mchango wao katika ajira na shughuli za kiuchumi ni mkubwa. Ushirikiano huu pia unajumuisha jitihada maalum katika kusaidia biashara zinazomilikiwa na wanawake na kuendeleza ushirikishwaji wa kijinsia, ikiwa ni sehemu muhimu ya mkakati wa IFC nchini Tanzania na Afrika,” alibainisha Sérgio Pimenta, Makamu wa Rais wa IFC Afrika.

IFC ina uhusiano wa muda mrefu na Benki ya CRDB. Mkataba huo wa makubaliano wa uwezeshaji kibiashara uliowekwa sahihi leo ni wa tano baina ya taaisi hizo, na ni sehemu ya kazi inayokua ya IFC nchini Tanzania kusaidia ukuaji wa biashara ndogo ndogo na kukuza uwezeshaji kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Afrika, Sergio Pimenta (kulia) wakitia saini mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 105 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo katika hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) akizungumza katika hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya mkopo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 105 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo katika hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam. kulia ni Makamu wa Rais wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Afrika, Sergio Pimenta.

ADVERTISEMENT

 

 

ADVERTISEMENT

 

 

 

 

 

 

Related

Tags: CRDB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .
HABARI

Mainstream Media Limited Waendesha Mafunzo Maalumu kwa Wakufunzi wa Vicoba  .

by I am Krantz
Aug 8, 2022
UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA
HABARI

UKRAINE YAISHTUMU RUSSIA KUSHAMBULIA KIWANDA CHA NYUKLIA

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI
HABARI

POLISI WATANO WAUAWA NA WASHAMBULIAJI

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU AGOSTI 08, 2022
HABARI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU AGOSTI 08, 2022

by Shabani Rapwi
Aug 8, 2022
ACHA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI
HABARI

ACHA KUNYONYA SEHEMU ZA SIRI WAKATI WA KUFANYA MAPENZI

by Shabani Rapwi
Aug 7, 2022
NMB Mshiko Fasta kuwanufaisha wakulima
HABARI

NMB Mshiko Fasta kuwanufaisha wakulima

by I am Krantz
Aug 7, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
July 2022
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Aug »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In